TRUMP KUFUTA SERA ZA OBAMA

 

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ametishia kufutilia mbali sera ya rais Barrack Obama ya kurejesha uhusiano kati ya Marekani na Cuba wakati atakapochukua madaraka Januari mwakani.

Trump amesema uamuzi huo utategemea utawala wa kikomyunisti mjini Havana, kuweka sera ambazo zitaimarisha hali ya maisha kwa raia wa nchi hiyo, na wale waliochukua uraia wa Marekani na wale wa Marekani.

Utawala wa rais Obama umejitahidi kurejesha uhusiano na utawala wa Havana, baada ya uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.

Trump amemtaja marehemu Castro kama kiongozi mkatili wa kiimla ambaye aliwakandamiza raia wake kwa miongo kadhaa.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments