Rais
Barack Obama wa Marekani amekutana kwa faragha na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani
kwa chakula cha jioni baada ya kuwasilii Berlin katika ziara yake ya mwisho
barani Ulaya akiwa rais wa Marekani.
Mkutano huo wa chakula cha jioni ulifanyika
katika Hoteli ya Adion ambayo iko karibu kabisa na eneo la kihistoria la
Brandenburg Gate mjini Berlin ambapo Obama na ujumbe wake watakuwapo hadi kesho
Ijumaa.
Haikuweza kufahamika kitu gani hasa viongozi
hao wawili wamekijadili juu kwamba yumkini masuala waliyojadili ni pamoja na
kuchaguliwa kwa Donald Trump katika uchaguzi wa rais kuchukuwa nafasi ya Obama
na mzozo wa Syria.
Mazungumzo zaidi yanatarajiwa kufanyika
baadae leo hii katika ofisi ya Kansela Merkel.Obama aliwahi kumpongeza Merkel
kuwa ni mshirika wa kuaminika na alitetea msimamo wake wa kushughulikia mzozo
wa wakimbizi ambao ulimgharimu kisiasa kwa kushuka kwa umashuhuri wake nchini
Ujerumani.
0 Comments