MEYA CHIMA, WANANCHI WA MTAMAA B SINGIDA ONDOENI WASIWASI

Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Chima (picha hii ni kutoka makitaba )
Wananchi wa kijiji cha mtamaa B wilaya ya Singida wametakiwa kuondoa wasiwasi wao kuhusu fedha za malipo ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi mtamaa B lenye ukubwa wa hekari 8 kwani swala hilo liko kwa mkurugenzi hivyo wajiandae kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hiyo

Meya wa manispaa ya Singida ambaye ndiye diwani wa kata hiyo ya mtamaa Bw. Mbua Chima amesema ingawa eneo hilo linahitaji kuongezwa hadi kufikia hekari 10 hadi 12 na kwamba tayari wanasubiri fedha kwa mkurugenzi zilizotokana na mapato ya soko la kijiji hicho ili waweze kumlipa mwananchi mwenye enero hilo

Aidha mwenyekiti wa kijiji cha mtamaa Bw. Hamisi Mwanja amesema wameamua kujenga shule katokana na changamoto ya umbali wanakotoka watoto wa kijiji chake kwenda kusoma shule ya Mtisi ambapo watoto wwengine hutembea zaidi ya kilometa mbili kufika shuleni hapo hali inayowalazimu kushinda na njaa wakiwa shuleni

Naye Bw. Zefania shaabani ambaye ni mzazi na mjumbe wa serikali ya kijiji cha mtamaa amesema jambo hilo wamelipokea kwa mikono miwili huku akisema watoto wao wamekuwa wakipata shida katika swala la elimu na ni lazima wajenge shule ili watoto wapate elimu kwani ni haki yao


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments