Emmanuel luhahula mkuu wa wilaya ya Iramba Mgeni rasimi mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel luhahula akilakiwa na diwani wa kata ya Shelui Hamisi Kinota . |
Timu ya Shelui |
Timu ya kinadada wa kijiji cha mtoa kata ya Shelui wilaya ya Iramba. |
MKUU
wa Wilaya ya Iramba,Mkoani Singida,amefungua tamasha la sanaa na michezo katika
Tarafa ya Shelui, wilayani humo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya hiyo
waendelee kujenga utamaduni wa kuibua vipaji vya wasanii wa sanaa na michezo
mbali mbali,itakayochangia kuleta hamasa na mshikamano miongoni mwao kwenye
maeneo yao.
tamasha
hilo la kumuenzi Baba wa Taifa,awali lilipangwa kufanyika Okt,14,mwaka
huu,lakini likasogezwa mbele kutokana na sababu mbali mbali,ikiwepo kupisha
shughuli zingine za kitaifa zilizojitokeza.
EMMANUELI
LUHAHULA ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, ametoa changamoto hiyo katika Mji mdogo
wa Shelui,wilayani Iramba alipokuwa akifungua Bonanza la Sanaa na michezo
lililoandaliwa na Madiwani wa tarafa hiyo,kwa lengo la kumuenzi Baba wa
Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
hata
hivyo licha ya kuwaagiza watendaji katika tarafa za Kisiriri,Ndago na
Kinampanda kuiga utamaduni ulioonyeshwa na tarafa ya Shelui,Mkuu huyo wa wilaya
amesisitiza pia kuwa kuna kila sababu za kuwa na timu ya wilaya hiyo kutokana
na kuamini kwamba kuna wapenzi wa michezo na wasanii katika wilaya hiyo.
awali
katika risala iliyoandaliwa na kamati ya maandalizi ya Bonanza la Sanaa na
Michezo na kusomwa na Mwajuma Rugambwa imeyataja manufaa huku mmoja wa
Waandaaji hao ambaye pia ni diwani wa kata ya Shelui,Hamisi Kinota akivifagilia
vyombo vya habari vilivyoshiriki kwenye ufunguzi huo.
katika
mchezo kati ya timu ya soka wanawake ya kata ya Mtoa na Shelui,Mtoa waliibuka
kidedea kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 yaliyopatikana kwa njia penalti na kwamba
mafanikio ya Bonanza hilo yametokana na mawazo yaliyotolewa na madiwani wa viti
maalumu tarafa ya Shelui,Jeniffer Miano na Rehema Balali kwa diwani wa Kata ya
Shelui,Hamisi Kinota.
0 Comments