Victor Mlotshwa
Theo Martins Kackson na Willem Oosthuizen |
Mtu mweusi nchini Afrika Kusini ambaye
alidaiwa kulazimishwa kuingia katika jeneza na wakulima wawili weupe kwa kupita
katika shamba lao amesema kuwa anahofia maisha yake.
Victor Mlotshwa alikuwa akizungumza nje ya mahakama ya mji wa
kaskazini mashariki wa Middelburg ambapo waliotaka kumshambulia waliwasilishwa
katika mahakama.
''Nilidhani wataniua'',alisema.
Kanda ya video ya dakika 20 iliorekodi kisa hicho imekuwa
ikisambaa katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani huko Middelburg anasema kuwa
ndani ya mahakama hiyo ,washtakiwa hao ,Theo Martins Kackson na Willem
Oosthuizen,walisimama wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini huku waandishi wa
habari na raia wakichukua picha zao.
Wameshtakiwa kwa kumteka nyara na kumshambulia kwa lengo
kumjeruhi vibaya.Hawajakubali ama kukana mashtaka hayo.
Wawili hao wanazuiliwa hadi tarehe 25 Januari huku waendesha
mashtaka wakisema kwamba walihitaji muda zaidi kuchunguza ,ikiwemo kuthibitisha
video hiyo.
Mamake bw Mlotshwa alijawa na hasira na kushindwa kujizuia
wakati wa kusikizwa kwa kwesi hiyo.Nje ya mahakama kulikuwa na kelele za
wafuasi wa vyama vikuu nchini humo huku #RacismMustFall ikisambazwa katika
mitandao ya kijamii.
0 Comments