Mussa Ramadhani Sima mbunge wa jimbo la Singida Mjini na mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Singida SIREFA. |
Rais John Magufuli leo amefanya
mabadiliko katika baraza la mawaziri na katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kama ifuatavyo:
Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko
hayo kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.
Taarifa hiyo imesema kwamba
nafasi ya Kangi Lugola inaenda kuchukuliwa na Mbunge wa Singida Mjini,
Mh. Mussa Ramadhan Sima.
Aidha Rais amefanya uteuzi wa Naibu
Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhumu wa Wizara hiyo ambapo,
Mbunge wa Morogoro Kusini Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.
Pamoja na hayo, katika mabadiliko
hayo madogo, Rais Mgufuli amefanya Uhamisho Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku
aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa
Uchukuzi.
Hata hivyo Balozi Kijazi amesema
tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye.
0 Comments