Uongozi wa klabu ya Simba umemkabidhi Shiza Kichuya tuzo
ya mchezaji bora wa mwezi September baada ya winga huyo kuisaidia klabu yake
kupata pointi 12 katika mechi nne alizocheza mwezi huo, matokeo ambayo
yameifanya Simba kuendelea kuongoza ligi.
Kichuya aliisadia Simba kwa kufunga magoli na kusaidia magoli mengine
kufungwa. Alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne alizocheza.
Umekuwa ni utamaduni wa Simba kutoa tuzo ya mchezi bora kila mwezi
ambapo wachezaji hupigiwa kura na mashabiki wa timu hiyo.
Mbali na tuzo hiyo, Kichuya pia alitangazwa mchezaji bora wa mwezi kwa
upande wa ligi kuu Tanzania bara.
0 Comments