Mfalme Mohamed VI wa Morocco akiwasili |
MFALME Mohammed VI wa Morocco amekubali
kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu katika makao makuu ya nchi mjini
Dodoma.
Hayo yamesemwa leo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla fupi ya
kusaini makubaliano mbalimbali ya kibiashara kati ya Tanzania na Morocco
iliyofanyika Ikulu mjini Dar es salaam.
Akizungumza mbele ya Mfalme huyo ambaye
alikuja nchini jana jioni, Rais Magufuli alisema kwamba alimuomba msaada wa
kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu mjini Dodoma, ombi ambalo
limekubaliwa.
Mfalme huyo aliwasili nchini nchini Oktoba
23, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Magufuli.
Alitua Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere mjini Dar es Salaam majira ya saa 11 Jioni na kupokewa na mwenyeji
wake, Rais Magufuli kabla ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi la
Jeshi la Wananchi Tanzania lililoandaliwa kwa heshima yake.
Leo jioni Mfalme Mohammed VI atashiriki dhifa
ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais Magufuli.
0 Comments