Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh Isaya Mwita |
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo amekiri kuwa
mtangulizi wake ambaye amefariki dunia, Didas Masaburi alifanya kazi kubwa ya
kuboresha miundombinu ya jiji hilo pamoja na kulitambulisha katika anga za
kimataifa.
Meya Mwita
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika safari ya mwisho ya kuuaga mwili
wa Marehemu Masaburi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Binadamu
anapokuwa ameondoka huwa tunazungumza mema aliyoyafanya katika jamii yetu. Mimi
Sikuwahi kufanya nae kazi lakini nimekuta kazi ambazo amefanya katika
halmashauri ya jiji,” amesema.
Ameongeza
kuwa “Moja ya mambo ambayo sitasahau niliyoyakuta aliyoyafanya katika utawala
wake ni kuuleta mradi wa DMDP uliolenga kusukuma na kutaka kuboresha maeneo ya
miundombinu ya DSM, ukiona kazi aliyoacha mimi ndio naendelea nayo sasa.”
Amesema
jambo lingine alilofanya Marehemu Masaburi enzi za utawala wake ni kuleta miji
mikubwa duniani kuja kuwekeza na kutoa misaada ya kimaendeleo nchini.
Miongoni
mwa majiji aliyoyataja Mwita ni jiji la Hamburg, Shanghai na Torotonto.
“Aliileta
hapa miji mikubwa duniani, mimi napata mialiko sasa katika nchi mbalimbali na
hii ni matunda ya jitihada zake katika kulitangaza jiji la Dar es Salaam na
Tanzania kwa ujumla.” amesema.
Pia Meya
Mwita amesema kuwa, Masaburi alifanikiwa kutoa mamlaka na madaraka ya
kiutendaji kutoka serikali kuu hadi serikali za mitaa.
“Alipokuwa
akiongolea dhana kubwa ya kutoa madaraka kutoka serikali kuu kuja serikali za
mitaahili, alikuwa anamaanisha. Jambo hili si jepesi kwa kuwa, halmashauri za
mitaa bila ya kuwa na nguvu kubwa haziwezi leta maendeleo mfano Kenya na Uganda
halmashauri zake zinauwezo na mamlaka ya kupanga maendeleo,” amesema.
Amesisitiza
kuwa “Japo hakufanikiwa kwa kiwango hicho mawazo yake yataishi na mimi kama
mrithi wake nitaendelea kuyaenzi.”
Marehemu
Didas Masaburi enzi za uhai wake aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT).
Viongozi mbalimbali wa serikali na maraisi wastafu akiwemo raisi Dr John Pombe Mgufuli |
0 Comments