Mkuu wa mkoa wa Singida mhandisi
Mathew Mtigumwe,amezishauri kamati shule za msingi na bodi za shule sekondari
kuanzisha utamaduni wa kujenga majengo ya ghorofa pindi zinapoamua kuongeza
majengo mapya
Amesema
baadhi ya shule za msingi zilizopo mjini Singida,zimeanzishwa miaka mingi
iliyopita wakati huo idadi ya wanafunzo ilikuwa ndogo lakini kwa sasa idadi ya
wanafunzi imeongezeka huku maeneo yaliyotengwa yakibakia yale yale.
Mhandisi
Mtigumwe ametoa ushauri huo juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa
vyumba vinane vya madarasa na matundu 20 ya vyoo vya shule ya msingi Nyerere
Shule
ya Nyerere inahitaji la vyumba vya madarasa,ni 35,vilivyopo ni 15 na
vinavyojengwa ni vinane.
Kutokana
na ukweli huo,mkuu huyo wa mkoa,amesema nafasi ya kuendelea kujenga majengo ya
chini haipo tena,hivyo alishauri kuanzia sasa ujenzi wa majengo mapya,uwe wa
ghorofa na si vinginevyo
0 Comments