Maafisa wa polisi nchini Uganda
wamewakamata vijana wawili waliokuwa wakimfanyia kampeni mgombea wa urais
nchini Marekani Donald Trump katika ubalozi wa Marekani mjini Kampala.
Mtandao unaounga mkono
serikali Chimp Riports umesema kuwa Vijana watano wa kundi la Young Democrats
nchini humo walijaribu kuingia katika ubalozi wa Marekani.
Gazeti la Daily Monitor
limechapisha ujumbe wa Twitter likionyesha picha za waandamanaji hao
Wafuasi hao wa Trump
waliambiwa maafisa wa polisi kwamba hawataruhusiwa ndani ya ubalozi kwa sababu
walikuwa hawajapata rukhusa kulingana na mtandao wa Chimp Report
Trump katika manifesto
yake alisema kuwa atakabiliana na marais waliohudumu kwa muda mrefu kutoka
Afrika akiwemo rais Museveni.
0 Comments