Kwenye mechi ya marudiano ya fainali mjini
Alexandria, Zamalek walipata ushindi wa 1-0 Jumapili lakini haukutosha kwani
walikuwa wamelazwa 3-0 na Sundowns mechi ya kwanza mjini Atteridgeville
Jumamosi wiki iliyopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya
Afrika Kusini kushinda kombe hilo.
Mara yao ya mwisho kufika fainali ilikuwa
mwaka 2001 walipolazwa na mahasimu wakuu wa Zamalek, Al Ahly.
Zamalek walipata bao lao la pekee Jumapili
dakika ya 62 kupitia Stanley Ohawuchi.
Kipa wa Sundowns Denis Onyango aliumia
kwenye goti dakika ya 12 na akaondolewa uwanjani kwa machela dakika ya 28.
Wayne Sandilands alichukua nafasi yake.
Maafisa wa Misri, ambao awali walikuwa
wamesema ni mashabiki 20,000 pekee wangeruhusiwa uwanja wa Borg El Arab kwa
sababu za kiusalama walibadilisha msimamo wao na kuruhusu theluthi tatu ya viti
kwenye uwanja huo unaotoshea mashabiki 86,000 kujazwa.
0 Comments