Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ametatilisha hukumu ya wafungwa zaidi ya elfu mbili ambao walikuwa wamehukumiwa
kifo.
Rais amebadilisha hukumu hiyo na sasa wafungwa hao 2,747
watatumikia hukumu ya maisha jela.
Wahalifu wamekuwa wakihukumiwa kifo Kenya lakini hakuna
aliyewahi kuuawa tangu miaka ya 1980.
Watetezi wa haki wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa hukumu
hiyo.
Baadhi ya wafungwa hata hivyo wamekuwa wakilalamika kwamba
hakuna tofauti ya hukumu ya kifo na maisha jela kwani mfungwa huwa anaishi jela
hadi kifo chake.
Rais Kenyatta pia amewaachilia huru wafungwa 102 waliokuwa
wakitumikia vifungo virefu.
Alhamisi wiki iliyopita, Rais Kenyatta alikuwa amewaachilia huru
wafungwa takriban 7,000 wa makosa madogo madogo au waliokuwa wanakaribia
kumaliza kutumikia vifungo vyao, na ambao walikuwa wameonyesha dalili za
kubadilisha tabia.
0 Comments