MWANDISHI WA CHANNEL TEN ANUSULIKA KATIKA AJALI

Basi la abiria la NAJIMUNISA lililokuwa likitokea Bariadi kuelekea Dar limepataajali na kupinduka Iguguno wilaya ya  Iramba  mkoani Singida mchana wa leo sep 27 akiwemo mwakilishi wa kituo cha luninga cha chanel ten Bariadi Pascal michael aliyekuwa akielekea jijini dar.

akizungumza na Katemana1.blog kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kupata matibabu katika kituo cha afya iguguno amesema kuwa basi hilo lilipata itilafu na kuyumba na kuanguka dereva wa basi hilo ametoroka hakuna mtu aliyepoteza maisha ila majerui wa tatu ndiyo wapo katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Pascal michael akitoka kuchukua begi lake akiongozana na abiria mama mwenye mtoto mgongoni.

Baada ya kupata matibabu abiria wengine walipandishwa kwenye basi la Simiyu na kuendelea na safari jioni ya leo akiwemo Pascal.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments