WAUGUZI WATUNUKIWA HESHIMA SINGIDA KWA MCHANGO WAO KATIKA SEKTA YA AFYA

 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Johanfaith Kataraia akiongea katika Siku ya wauguzi kwa niaba ya katibu tawala Mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Victorina Ludovic amewapongeza waudumu kwa kazi nzuri wanayofanya.

Israel Peter Mwenyekiti wa chama cha wauguzi (TANNA)Mkoa wa Singida akiongea katika siku hiyo ya wauguzi.

Wauguzi wakila kiapao cha utii katika siku hiyo ya wauguzi ngazi ya Mkoa wa Singida

SINGIDA

Katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani kwa ngazi ya Mkoa wa Singida, serikali imesisitiza kutambua na kuunga mkono mchango wa wauguzi kama mhimili mkuu wa huduma za afya nchini. Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Manispaa ya Singida, yakiongozwa na kaulimbiu ya mwaka huu: "Uuguzi: Nguvu ya Mabadiliko Duniani."

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Johanfaith Kataraia, alisema kuwa wauguzi na wakunga wanachukua asilimia 60 ya watumishi wa afya, huku asilimia 80 ya kazi zote katika sekta hiyo zikitekelezwa na wauguzi.

“Serikali ipo bega kwa bega na wauguzi katika kuimarisha taaluma hii adhimu. Tunaendelea kuboresha miundombinu ya afya ili kuhakikisha wauguzi, wagonjwa na wateja wanahudumiwa katika mazingira salama na rafiki,” alisema Kataraia.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovic, aliwapongeza wauguzi kwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kujitolea, akisisitiza kuwa mara nyingine wauguzi huchukua jukumu la usimamizi wa mali za serikali kwa uaminifu mkubwa.

Katika risala yake, Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Singida, Bi. Joycey Muyenjwa, alieleza historia ya Florence Nightingale — muasisi wa taaluma ya uuguzi duniani — na mchango wake katika kuweka misingi ya huduma bora ya afya kwa upendo, huruma na maadili ya kazi.

Maadhimisho haya yalipambwa na burudani, maonyesho ya kazi za wauguzi, upimaji wa afya kwa wananchi, na mijadala juu ya namna ya kuinua zaidi taaluma ya uuguzi nchini, sambamba na kuendeleza mazingira bora ya kazi kwa wauguzi.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments