MAUTUKIO YA PICHA ZA RAIS J.P.M AKIZINDUA KIWANDA CHA MOUNT MERU MILLES SINGIDA

Nje ya kiwanda hicho kilichopo maeneo ya FFU manispaa ya Singida  ndipo Mh Rais John Pombe Magufuli alipozindulia kiwanda hicho.
Wenyeviti wa Halmashauri ya wilya za mkoa wa Singida Kushoto ni Mstaiki meya wa Manispaa ya mji wa Singida Mh Mbua Chima huku wakwanza mbele ni Mh AllyMinja Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Itigi .
Wabunge wa Mkoa wa Singida wakicheza ngoma ya asili ya Wanyaturu kulia ni Mh Matha Mlata , Mh Asharose Matembe   viti maalum Mh Mussa Sima Mbunge wa Singida mjini na Mh J.Monko mbunge mpya wa Singida vijijini (DC).

Wafanyakazi wa Mount meru.


Kulia ni Afisa mausiano wa kiwanda cha Mount Meru katikati ni mfanya biashara kushoto ni Leonard Manga wa TBC
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akisakata Rhumba kwa furaha .
MC Mavunde akisherehesha 
Mh Rais J.P.Magufuri akiwasili katika viwanja vya kiwanda cha Mount Meru.


Rais John J.Magufuli akiimba wimbo wa Taifa katikati ni mkurugenzi wa kiwanda cha  Mount Meru   
Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida.
Wakuu wa wilaya za Singida .

Mbunge wa Jimbo la Singida Mh Mussa Sima alipata fulsa ya kuongea na wananchi waliyo udhulia  katika uzinduzi huo.
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli akipata  maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Mount Meru wakati akielekea kukata utepe.




Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa .
Rais Dr John Pombe Magufuli akihutibia hadhala kabla ya uzinduzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupandisha kodi kwa waingizaji wa mafuta ghafi ya chakula kutoka nje ya nchi.
Akizindua kiwanda cha kusindika mafuta cha Mount Meru Milles cha mjini Singida Rais Magufuli amesema hatua hiyo itawezesha wawekezaji wa ndani wa viwanda vya mafuta ya chakula kupata soko.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati Serikali ikifanya maandalizi kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/19.
Amesema anafahamu mchezo mchafu unaofanywa na waagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuua soko la ndani la mafuta ya chakula.
Rais Magufuli amesema wanachofanya wanaagiza mafuta kwa kisingizio kuwa ni (mafuta ghafi) yanayohesabika kama ni malighafi


Amesema kwa kisingizio hicho, TRA na watu wengine hawawatozi kodi na wanapoyafikisha nchini waagizaji hao huyaweka kwenye madebe na kuyauza hivyo kutengeneza faida kubwa.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments