Mkurugenzia Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Singida wa (SUWASA)
Sebastian Warioba akiongea na wanahabari Ofisini kwake.
wananchi na wakazi wa Karakana Manispaa ya Singida wa sikitishwa na vitendo vya wizi wa mita za maji unaoendelea sasa.
SINGIDA:
Wakazi wa
Kata ya Karakana, Manispaa ya Singida, wameibua kilio kwa Serikali na Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) kufuatia wimbi la wizi wa mita za
maji linaloendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.
Wakizungumza
na wanahabari, wakazi hao wamesema wizi huo umesababisha ukosefu wa huduma ya
maji kwa muda mrefu, hali inayowalazimu kutafuta maji mbali na makazi yao.
Wameomba hatua kali zichukuliwe haraka ili kukomesha vitendo hivyo.
“Huduma ya
maji ikikatika kwa sababu ya wizi wa mita, maisha yanakuwa magumu. Tunahitaji
suluhisho la haraka,” alisema mkazi mmoja wa Karakana.
Mkurugenzi wa
SUWASA Singida, Sebastian Warioba, amesema kuwa jumla ya mita 80 za
maji zimepotea kutokana na wizi huo. Ameeleza kuwa mamlaka hiyo inashirikiana
na Jeshi la Polisi kuwabaini wahusika.
Aidha,
SUWASA imetangaza zawadi ya shilingi laki tano kwa yeyote atakayetoa taarifa
zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa wizi wa mita hizo.
“Tunataka
kushirikiana na wananchi kumaliza tatizo hili. Taarifa zote zitapokelewa kwa
usiri mkubwa,” amesema Warioba.
0 Comments