Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga akiongea katika kikao hicho
Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki kutoka Singida akiongea katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa VIP Nanene jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa waSingida Mheshimiwa Halima Dendego amewakaribisha wawekezaji wakubwa na wadogo
kwenda kuwekeza katika mkoa huo kwa sababu tayari imeweka mazingira mazuri kwa
mtu au Kampuni kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo Viwanda, Kilimo, Madini
na Utalii.
Akizungumza kwenye
Kongamano la Uwekezaji lililojumuisha wawekezaji
mbalimbali kutoka
ndani na nje ya nchi katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika
Jijini Dodoma, Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewahakikishia
wawekeza watakaowekeza kwenye mkoa wake kuwa watakuwa wamechagua mkoa sahihi wa
kuwekeza kwa sababu upo kati kati ya nchi na miundombinu ya usafiri ni mizuri.
Mkuu huyo wa Mkoa
amesema kuwa anataka kuona mkoa ya Singida unakuwa mkoa wa kwanza nchini kwenye
idadi kubwa ya wawekezaji kama hatua ya kukuza uchumi wa wananchi na wa Taifa
kwa ujumla kupitia fursa za uwekezaji.
Kwa Upandewake,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kufungua Kongamano hilo la uwekezaji, amesema kwa
Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki katika uimarishaji wa uwekezaji hasa
katika sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa sababu zinamchango mkubwa katika
kuinua uchumi wa wananchi na wa Taifa kwa ujumla.
Profesa Mkumbo amesema kwa sasa Serikali imefanya marekebisho makubwa ya sera na sheria za
uwekezaji nia ikiwa ni kuondoa vitendo vya ukiritimba ambavyo vilikuwa
vinakwamisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mchakato huo unaenda sambamba na upunguzaji wa utitiri wa baadhi ya Taasisi mbalimbali
za umma ambazo zingine ni legevu na zimekuwa kiwango katika masuala ya
uwekezaji.
Kongamano hilo
limehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu na Balozi wa Kilimo nchini Mizengo
Pinda.
0 Comments