Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Ramadhani Ighondo ameongoza wananchi na wakazi wa kata ya Mtinko katika zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Malolo kwa ushirikiano na mkurugenzi taasisi ya TAA Suphiani Juma.
Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Ramadahani Ighondo tarehe 06/08/2024 ameongoza zoezi la Upandaji Miti 800 katika shule ya Msingi Malolo iliyopo Kata ya Mtinko. Mhe Mbunge amepanda miti hiyo kama sehemu ya kampeni ya "Singida ya Kijani inawezekana" inayoratibiwa na Shirika la TAA wakishirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)
Akiongea wakati wa zoezi hilo Mhe. Ighondo amewataka wananchi waitunze miti hiyo kwa ajili ya manufaa yao kwa Sasa na hapo hasa katika utunzaji wa mazingira,na amemshukuru Mkurugenzi wa Shirika la TAA Ndg Suphian Juma Nkuwi kwa nia yake ya kuhakikisha Singida inakuwa ya Kijani kupitia Kampeni hii n amemuomba miti mingine mingi ipandwe kwenye Taasisi mbalimbali Jimbo la Singida Kaskazini.
Mkurugenzi mtendaji wa TAA Ndg Suphian ameridhia ombi la Mbunge kuleta miti mingi jimboni kwake ipandwe kwenye Taasisi mbalimbali ili kutunza mazingira
0 Comments