HII NDIYO SINGIDA BLACK STARS ON BIG DAY

 










NAIBU meya  manispaa ya Singida Mhe Geoflya Mdama,amesema kuwa mkoa wa Singida utaendelea kusapoti michezo mbali mbali, pamoja na mambo mengine,mkoa  unaweze kutangazwa ndani na nje ya nchi kupita michezo.

Naibu huyo ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukagua timu ya Singida Black Star  na timu kutoka Burundi ,Aigle noir.Mchezo  huo umefanyika uwanja wa Leti mjini Singida.

Ili kufikia lengo amewataka vijana wajitokeza kwa uwingi kuonyesha vipaji vyao,waweze kuendelezwa kwa faida yao na mkoa  kwa ujumla.

“Tunatarajia mbele ya safari,mkoa  wetu utakuwa umetangazwa  zaidi pengine zaidi ya Yanga na Simba za Dar-es-salaamu”,Mdama amesisitiza ambaye alimwakilisha meya  wa manispaa ya Singida Yagi Kiaratu.

Katika hatua nyingine,timu ya Singida Black star,iliichapa Aigle noir ya Burudi, goli moja kwa bila.Goli hilo lilifungwa na Joseph Guede katika dakika ya 72 kipindi cha pili.

Hata hivyo,viongozi wa maandalizi ya hafla hiyo iliyotumika Singida Blach Star kutangaza wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi likongozwa na kocha mkuu Patick Ausseams,walifuta viingilio hivyo, na wapenzi kuingia bure kuangalia mchezo huo.

Ni  jukwaa kuu, ndilo lilijaza wapenzi wengi  wa soka,huku jukwaa la mzunguko,likiwa na watazamaji wachache mno.

Ayubu Yangu wa Singida Black  Star amewapa  matumaini wakazi wa mkoa wa Singida,kwamba waondoe hofu timu inaenda kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu, inayotarajiwa kuanza agosti 18 mwaka huu.

Singida itaanza kucheza na timu ya Mbeya  city ambayo mchezo huo  utafanyika jijini Mbeya  agosti 18 mwaka huu.Wapenzi wa soka mkoa wa Singida,watarajie pointi tatu.

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments