BONANZA LA VIJANA WA KATA 13 SINGIDA MASHARAIKI.

 


Mbunge wa vijana kupitia viti maalum Mhe Nusrat Hanje akiongea na wanamichezo kutoka kata 13 za jimbo la Singida Masharaiki katika viwanja vya sekondari ya Mungaa kata ya Makiungu.

Diwani wa kata ya Makiungu Mhe John Mathias akimshukuru Mbunge Nusrat Hanje kwa kuwakutanisha vijana kwa lengo la kuhamashisha kujitokeza kwenye uchaguzi.

Mwenyekiti wa  Makiungu akitoa neno la uzinduzi wa  bonanza hilo kwa mgeni rasimi .

Wito umetolewa kwa vijana kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la mkazi sambamba na kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Vijana viti maalum wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Nusrat Hanje katika bonanza la Vijana lililo wakutanisha vijana kutoka kata 13 za jimbo la Singida Mashariki Wilani Ikungi.

Hanje amesema kuwa vijana wananafasi pia ya kuongoza katika ngazi mbalimbali nchini ikiwemo nafasi za mwenyekiti na maeneo mengine.

Awali akizindua Bonanza hilo lililo fanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mungaa iliyopo Makiungu,Mwenyekiti wa Mtaa huo Hamisi Haji amesema kuwa michezo ni Afya michezo ni kazi kama kazi zingine huku akimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano kwa sapoti kubwa anayoitoa katika Michezo Nchini

Naye Diwani wa Kata ya Makiungu Mhe.John Mathias akiongea kabla ya kumkaribisha Mbunge  amempongeza Mbunge huyo kwa kuwakutanisha vijana kwa pamoja kupitia michezo mbalimbali iliyofanyika katika bonaza hilo.

Katika bonanza hilo Michezo mbalimabli ilikuwepo ikiwamo Draft,kukimbia na yai,kukimbia na Gunia,Mpira wa Pete(Netball),kufukuza kuu na mpira wa miguu,huku timu zote kutoka kata 13  zikipatiwa vifaa mabaliombali vya michezo zikiwamo Jezi na Mpira.

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments