Meneja wa kanda ya kati kutoka kampuni ya Taifa Gesi Baraka Lesso akitoa malezo mafupi juu ya kampuni hiyo ya Taifa Gesi.
Na mwandishi wetu
Watumiaji wa nishati ya gesi wametakiwa kuwa makini wanapotumia nishati hiyo kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kulipuka kwa gesi itakayopelekea kuungua kwa vitu mbalimbali.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa nishati hiyo Mkoa wa Singida baada ya Baraza la watumiaji wa huduma ya nishati na maji mkoani hapa EURA CCC kutembelea kwa lengo la kujifunza ili kuja kuwaelimisha wananchi.
Akitoa baadhi ya tahathari ya namna ya matumizi ya gesi meneja wa Kanda ya kati kutoka kampuni ya Taifa gesi Bakari Lesso amesema ni vyema wananchi wanaotumia nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali kuwa makini.
Aidha kwa upande wake msimamizi wa kituo cha kampuni ya Taifa gesi Singida Said Aman ametoa angalizo na namna ya ubebaji wa mitungi ya gesi ili isilete madhara kwa mtumiaji.
Naye mwenyekiti wa
kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji mkoa wa Singida Said Mtoro
anaeleza lengo la uwepo wa EURA CCC.
0 Comments