Diwani wa Kata ya Mwanga Mhe Mohamed Hamisi Juma akitoa Taarifa ya Miradi Mbalimbali ya Maendeleo iliyotekelezwa katika kata hiyo kupitia fedha za Serikali zilizotolewa.
Mkuu wa Mkoa Singida akimpongeza diwani wa Kata hiyo kwa usimamizi mzuri wa shughuli za Maendeleo na Miradi ya Serikali katika kata yake.Meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego (katikati) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata(kulia) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Bethar Nakomolwa kwa pamoja wakifuatilia taarifa ya Diwani wa kata hiyo Mohamed Hamisi Juma.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali akiongea na wananchi wa kata ya Mwanga ikiwa ni katika ziara ya kamti ya Siasa ya Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Halima Dendego alipata fursa ya kuongea na wananchi wa kata hiyo ya Mwanga.
Mgeni rasimi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata pamoja na mambo mengine ametoa pongezi kwa Polisi kata kwa kazi nzuri ya usimamizi mzuri wa mali na usalama wa raia.
Na Mwandishi wetu
Wananchi
wa kata ya Mwanga Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida wameishukuru serikali kwa
kuwaondolea kodi za matrekta na kuwawezesha kununua jambo ambalo limewanufaisha
katika sekta ya kilimo.
Hayo
yameelezwa na diwani wa Kata hiyo Mohamedi Hamisi Juma wakati wa mkutano wa
hadhara wa kamati ya siasa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Singida uliofanyika
katika Kijiji cha Kidarafa.
Mohamedi
ameeleza kuwa pamoja na serikali kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo
miundo mbinu ya barabara, elimu na Afya pamoja na kuwawezesha wakulima kununua
matrekta ambayo yamewasaidia na kuwarahisishia shughuli za kilimo.
Aidha
mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amesema atawashughulikia wote wanaotoa
lugha za matusi kwa serikali kwa kuwabeza wanawake kuwa hawawezi kuwa viongozi
na kuwatolea maneno machafu.
Naye
mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida Martha Mlata amewaasa wananchi hao
kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kumshukuru mkuu wa Mkoa kwa kuahidi
kuwawezesha wananchi hao katika shughuli zao za kilimo.
0 Comments