Ofisa Mahusiano Mradi wa Bomba la Mafuta Abbas Abraham akitoa maelezo mafupi juu ya Mradi huo.
SINGIDA
Na
Mwandishi Wetu
Waandishi
wa Habari Mkoani Singida wametakiwa kuendelea na utoaji Elimu kupitia taaluma
ya Habari juu ya Miradi mbalimbali ya
kimkakati inayoendelea kufanyika Nchini ukiwamo Mradi wa Bomba la Mafuta unaoendelea
na Ujenzi Mkoani hapa.
Ofisa
Mahusiano ya jamii wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Chongoleani Tanga Josephat Kanyunyu amewaomba waandishi wa Habari kupitia
taaluma yao kutoa taarifa zinazoeleza umuhimu wa mradi huo ili wananchi waweze
kuutambua kwa kina.
Ofisa
huyo ametoa rai hiyo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji na hatua iliyofikia
ya mradi huo katika semina ya waandishi wa habari Mkoa wa Singida yenye lengo
la kuwajengea uwezo pamoja na kupata taarifa sahihi za mradi huo wenye kambi
yake mkoani hapa.
Aidha
ameeleza hatua ambazo zimefanyika mpaka sasa kwa wananchi waliopisha mradi huo
ikiwa ni pamoja na fidia.
Kwa
upande wake Ofisa Mawasiliano wa Mradi huo nchini Tanzania, Abbas Abraham
amewaeleza Waandishi hao kuwa mradi huo umefanikiwa kukwepa athari za
kimazingira na kijamii.
Amesema
mradi umechukua maeneo ya wananchi takribani 9,000 kutoka katika mikoa yote
ambayo mradi umepita na wamekwisha lipwa fidia.
Hata
hivyo wanahabari hao wametoa wito kwa wasimamizi wa mradi huo kuwashirikisha
Waandishi wa Habari ili wawe na taarifa sahihi na kuifahamisha jamii kuhusu
mradi huo wenye manufaa kwao na Taifa kwa ujumla.
Mradi
wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda umepita katika Mikoa ya Kagera,
Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Tanga.
0 Comments