MKAZI wa Kitongoji cha Kibaya Kijiji cha Nsongambele Kata ya Ndago Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Juma Shabani (80) amekutwa amekufa asubuhi na Mkwe Tatu Selemani nyumba anayolala alipoona miti ya uzio wa zizi la ng’ombe haujaondolewa akatia shaka akaenda anakolala mume wake kujua kilichomfanya asifungue miti ya zizi la ng’ombe.
Imeelezwa, mke wake Tatu Selemani alipofika kwenye mlango wake
alikutana na damu, roho ikamruka akabaini mume wake Mzee Juma amekufa, amekatwa
kichwa upande wa kushoto na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni shoka.
Akitoa habari hizi kwa simu ndugu wa karibu (jina tunalo)
amesema tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita usiku wakati watu
wamelala na mzee Juma akiwa amelala kwenye nyumba nyingine.
Mtoa habari amesema Mzee Juma aliingiliwa usiku na watu wasiojulikana
akiwa amelala kwenye nyumba yake isiyokuwa na mlango akakatwa kichwa upande wa
kushoto juu ya sikio na chini ya sikio kwenye shavu hadi ndani ya ulimi kupitia
meno yake, alikatwa pia kisogoni na hasa ndicho kilichomfanya ashindwe kupiga
kelele.
Habari zinasema Tatu Selemani alipofika nyumbani anamolala mume
wake alikuta damu, akapiga kelel kwa nguvu Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibaya
alifika akiwa na majirani zake Ramadhani Buko, akasaidia kutoa taarifa kwa
viongozi wa kijiji na kata, walifika na kuhuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsongambele Martin Manase amesema
amezipata taarifa hizo za tukio hilo asubuhi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji
cha kibaya Ramadhani Buko na alipofika na kuhudia tukio hilo akatoa taarifa
Polisi Ndago na Wilayani Iramba.
Polisi walipofika wakafuatana na Waganga kushuhudia tukio hilo
na katika uchunguzi wao walibaini mzee Juma Shabani alikufa kutokana na maumivu
ya majeraha ya kukatwa kichwa na kitu chenye ncha kali kilichosimama wima
kinachodhaniwa kuwa ni shoka hata hivyo sababu za kuuawa kwake hazikufahamika
na waliomuua bado hawafahamiki mpaka sasa.
Habari kutoka familia yam zee huyo zinasema Mzee Juma Shabani
aliingia kitongoji cha Kibaya kijiji cha Nsongambele wilayani Iramba mwaka 1962
akamiliki eneo kubwa la kilimo na mifugo anawa watoto na vijukuu na alikuwa ana
mahusiano mazuri na wananchi wenzake na viongozi wa eneo hilo.
Polisi imewashikilia watu wanne akiwepo mke wake Tatu Jumanne
kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo, Polisi wanaendelea na uchunguzi
wao ili kujua kisa cha mzee huyo kuuawa.
0 Comments