Na Mwandishi wetu (w) Ikungi
KUMEKUWA na kundi dogo la fisi wanao zunguka usiku
kwenye makazi ya watu kitongoji cha Mrama Kijiji cha Musimi Kata ya Sepuka
Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida wamekula mbuzi,kondoo na mbwa na kutishia
maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mrama
Athumani Kijanga amethibitisha kuwepo kwa kikundi cha fisi kwenye eneo lake
wiki mbili sasa na tayari wamekula mbuzi 2 kondoo 1 na mbwa 1 lakini hakuna mtu
aliye ripoti wakushambuliwa na fisi japo kuwa watu kadhaa wamekutana na fisi
usiku.
Fisi hao ambao inasemekana kuonekana kwenye makazi
ya watu saa 12:00 jioni na asubuhi saa 12:00 amesema kuwa wanyama hao wanatashia amani kwa wakazi wa eneo hilo hasa wakulima mashambani kwenye mashamba ya Mtama,uwele na alzeti mkazi wa kijijini hapa Hamisi Saidi alitaka kung’atwa na fisi shabani kwake.
Habari zilizopatikana kutoka kitongoji hicho
cha Mrama zilizotolewa na mmoja wapo wa wakazi wa eneo hilo Antony Jakobo zinasema
watoto wake juzi saa 12:00 jioni wali kwenda kuchota maji mbugani wakati
wanarudi wakakutana na fisi akifukuzwa na kunguru wakalitupa galoni la maji
wakakimbia fisi huyo akaenda kulichukua galoni hilo kwa meno yake akaishia nalo
vichakani lakini baadae alikimbilia kwenye mashamba na akutokomea.
Kwa mujibu wa Antoni Jakobo fisi hao wamekula mbuzi
mbili kwenye mji wa Juma Omari, wamekula Kondoo mmoja kwenye mji wa Miraji Juma
na kwenye mji wa Juma Wawa wameondoka na mbwa wake na Hamisi Saidi alikutana na
fisi saa 3:00 usiku wakiwa nane akakimbia akiogopa kushambuliwa na fisi hivyo
ni wazi kuwa fisi waka sasa kwenye maeneo ya watu wakisaka chakula.
Afisa Mtendaji Kata ya Sepuka Abella Kibanda katika mahojiano mafupi juu ya kuwepo kwa wanyama hao
kwenye makazi ya watu kitongoji cha Mrama amesema ni kweli fisi wapo katika
eneo hilo la Mrama wahitokea kwenye hifadhi ndogo za vijiji wanadaiwa wamekula
mifugo ya watu na kutishia maisha ya watu lakini ofisi yake bado haina taarifa
rasmi hivyo anashidwa kuelezea vizuri.
Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA)
imetoa wito kwa viongozi wote wa vijiji vilivyopo kwenye hifadhi kubwa na
hifadhi ndogo za vijiji walipo wanyama hawa fisi mara tu wanapoanza kuonekana
kwenye makazi ya watu kushambulia mifugo na kutishia maisha ya watu ni muhimu
watoe taarifa mapema ofisi za viongozi wa Kata na Vijiji na zaidi ofisi za
wanyamapori zilizokaribu ili udhibiti ufanyike kabla madhara makubwa
hayajafinyika.
=MWISHO=
0 Comments