Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari za Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaabani Matwebe Akiongea na Wanahabari juu ya Mkutano huo.
Jumuiya ya Wanahabari wa
Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na Shirikisho la
Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imeandaa Kongamano la
Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20/5/2024
kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti JUMIKITA,
Shaaban Matwebe alisema Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi
ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa.
“JUMIKITA inapenda
kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili uandishi
wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia
mitandao hiyo. Pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya
miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na
maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani. JUMIKITA inawakaribisha wote
kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu”,alisema Matwebe.
Alisema mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao
ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na
changamoto ili kutoa mchango wa kiuendeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na
mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya
kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa
taarifa (information economy).
0 Comments