Mwenyekiti wa jumuiya ya Wzazi mkoa wa Singida Bertha Nakomolwa akiongea na wakazi wa kata ya Mukulu Wilayani Iramba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa
wa Singida ndugu Bertha Nakomolwa
amefika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba Maxhi 3,2024 kwa lengo la kusalimia
na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Mwenda na
wataalamu mbalimbali kwa namna wanavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
"Kwa niaba ya kamati ya
utekelezaji Mkoa tunampongeza Mkuu wa Wilaya ya Iramba kwa namna anavyotekeleza
Ilani kwa kuhakikisha miradi ya
Maendeleo inakamilika kwa wakati akishirikiana na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba" -
Alisisitiza Mwenyekiti wa Wazazi Bertha Nakomolwa
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya
ya Iramba Warda Obathany kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba,amewashukuru
Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa kwa Salamu zao za pongezi kwa Mkuu wa
Wilaya ya Iramba.
"Nimepokea salamu zenu za pongezi na nitazifikisha na ninawaahidi
tunashukuru mahusiano ya Viongozi wa Serikali na Chama ngazi ya Wilaya ni
mazuri Sana na tutaendelea kudumisha uhusiano huo". - Amesema Katibu
Tawala Wilaya.
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Singida amefanya ziara na Wajumbe w
Kamati ya Utekelezaji Mkoa kwa ;lengo la kufungua maadhimisho ya Wiki ya Wazazi
inayokwenda sambamba na utoaji elimu ya malezi, utunzaji mazingira, ushiriki wa
wanaCCM kwenye uchaguzi wa Serikali za
mitaa
0 Comments