Mkurugenzi wa Summaco Eng Co.Ltd Fenny Mashanjala akiongea katika maafali ya shule ya Msingi Misuna.
Mwenyekiti wa kamati ya Shulea ya Msingi Misuna akiongea na wazazi juu ya Shulea.
Mkuu wa Shule ya Msingi Misuna Karoli Urassa akitoa taarifa fupi ya shule hiyo.
SINGIDA
Waalimu na
uongozi wa Shule ya Msingi Misuna iliyopo Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida,
wamepongezwa kwa mchango wao mkubwa katika malezi na elimu bora ya watoto.
Pongezi hizo
zimetolewa na Mdau wa Maendeleo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sumaco Engineering
Company Ltd, Fenny Msahanjala, wakati wa sherehe ya mahafali ya Darasa la Saba
shuleni hapo.
Mashanjala
alisema licha ya changamoto zilizopo, bado ni muhimu kuendelea kuwafundisha
wanafunzi siyo tu masomo darasani, bali pia maadili ya Kitanzania ili wawe raia
wema na wenye maadili mema.
Aidha, baada
ya kushuhudia igizo lililooneshwa na wahitimu likiwa na maudhui ya harusi na
wapambe wao, Msahanjala alitoa angalizo kwa walimu na wazazi kuhakikisha michezo
ya watoto inazingatia maadili na umri wao.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Karoli Urassa, alieleza kuwa shule ya Misuna
kwa sasa ina wanafunzi 1,890, lakini ina walimu 26 pekee na madarasa 18, hali
inayosababisha upungufu mkubwa wa rasilimali za ufundishaji.
Aidha,
aliongeza kuwa shule hiyo ina madawati 330 pekee kati ya mahitaji ya madawati 630,
na pia walimu hawana vyoo vya matumizi yao. Alitoa wito kwa serikali na wadau
wa elimu kushirikiana kutatua changamoto hizo.
Awali,
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Elimboto Majengo, alihimiza wazazi kuchangia
chakula kwa ajili ya wanafunzi pamoja na kushiriki katika ununuzi wa madawati
ili kuimarisha ufaulu wa wanafunzi.
Sherehe hiyo
ilihudhuriwa na wazazi, walimu pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu
mkoani Singida.
0 Comments