Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akiongea na Askali hao baada ya Kuhitimu Mafunzo yao.
Na Mwandishi wetu
Iramba -Singida
Askari 90 wa Jeshi la Akiba, wakiwemo wanaume 62 na wanawake
28, wamehitimu mafunzo ya zaidi ya miezi minne ya mgambo yaliyofanyika katika
Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Akifunga mafunzo hayo Agosti 26, 2025, Mkuu wa Wilaya ya
Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda, aliwapongeza wahitimu kwa nidhamu na kujituma
kwao hadi kufanikisha kuhitimu mafunzo hayo. Aliwataka kuwa mabalozi wa amani
na uzalendo katika maeneo yao.
Vilevile, DC Mwenda aliwashukuru viongozi wa Kijiji cha
Kitukutu kwa ushirikiano wao uliowezesha mafunzo kufanyika kwa mafanikio
makubwa. Amesisitiza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuwapa kipaumbele vijana waliopitia
mafunzo ya mgambo, ikiwemo nafasi za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
na majukumu mengine ya kitaifa na kijamii.
Kwa upande wake, Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Iramba, SSGT
Omari Jabu Kidawa, alisema jumla ya vijana 90 walijiunga na mafunzo hayo,
ingawa 11 walishindwa kuhitimu kutokana na utoro.
Aliongeza kuwa masomo waliyofundishwa yamelenga kuwajengea uzalendo, nidhamu, ukakamavu na utayari wa kushiriki kikamilifu katika majukumu ya kitaifa.
0 Comments