Na Mwandishi wetu.
MKAZI wa Kitongoji cha Kipimbi
Kijiji cha Nsonga Kata ya Kaselya wilaya ya Iramba mkoani Singida Masumbuko
Ramadhani (54) ameng’atwa na nyoka aina ya Kifutu kwenye mkono wake wa kulia
wakati aking’olea majani kwenye moja ya majaruba yake ya mpunga.
Akitoa habari juu ya tukio hilo ndugu wa karibu Ramadhani Shabani (Mzanzibar)
amesema tukio hilo la kung’atwa na nyoka aina ya kifutu lilitokea saa 3:00
asubuhi wakati Masumbuko aking’olea majani kwenye shamba la mpunga.
Ramadhani amesema wakati ndugu
yake anaingiza mkono kwenye maji ili ang’oe majani kwenye shina la mpunga
akamtoa pamoja na majani ghafla akamuuma na hii ni katika kujihami kwa nyoka
huyo.
Habari zinasema Masumbuko akaona
ameinua kitu kizito kikiwa pamoja na majani huku nyoka huyo akitaka
kujiviringisha kwenye mkono akakung’uta kwa nguvu akaachia akamtupa chini
lakini alishamung’ata kidole kikubwa, akamkata kwa jembe na akafa hapo hapo,
lakini mkono wake ulikufa ganzi halafu ukaanza kuuma na kuvimba.
Masumbuko kuona hali hiyo na
kukumbuka ubaya wa sumu wa nyoka huyo akaenda nyumbani haraka akaagiza pikipiki nakukimbizwa kituo cha afya Sepuka na baada ya maelezo yake waganga wa kituo
hicho wakamchoma sindano moja na dripu mbili za maji na vidonge.
Akizungumza kwa njia ya simu
baada ya kurudi nyumbani Masumbuko amesema kuwa “alimkamata
nyoka huyo akamchanganya na majani akaanza kumvingirisha ili amuume Zaidi
akamkungutia chini akaachia na kuanguka akachukua jembe akamkata kichwa
akamuua, alikuwa na urefu wa sentimita 43.
Masumbuko ameendelea kusema
kwanza kidole ilichoumwa kilikufa ganzi sehemu ya juu ya mkono ilianza kuuma
sana na kuvimba mkono wote, lakini akiwa hapo kituo cha afya sepuka akiendelea
na matibabu baadhi ya watu walimgusia kuwa sumu ya nyoka hutibiwa na dawa asili
na mganga mmoja Kijiji cha Italala.
Ameendelea kusema, siku
iliyofuata asubuhi mkono ulivimba na ukaanza kuuma akaenda kwa mganga wa tiba
asili Mzee Shabani Makonga alipofika akamchanja chale kidole chote na kumuwekea
dawa zake, akamtolea meno mawili, akampa dawa ya kunywa ili aitoe sumu iliyoko
tumboni lakini kwa njia ya kuharisha na akaharisha kwa siku 4.
Masumbuko amesema, baada ya
kuharisha kwa siku hizo 4 mfululizo sumu yote ilitoka, uvimbe ulipungua siku
hadi siku na kwisha kabisa na sasa unatumika kama kawaida kwa sababu a;ikuwa
anakula kwa kutumia mkono wa kushoto.
Jamii nyingi zinahitaji kufahamu
Zaidi suala la watu kuumwa na nyoka na kutambua kile wanachopaswa kufanya
mapema kuhusu tiba zake huku mifumo ya afya nayo ikijengewa uwezo wa kutosha
kutoa tiba kamili za sumu za nyoka “Venon” hasa vijijini waliko watu wengi na
nyoka wengi.
Mkazi moja wa Kijiji cha Msungua
Amina Jingi aliumwa na nyoka shambani mwake akivunja mahindi ya kuchoma, aliona
kitu kikali kikimchoma mguuni akahisi mwiba alipoangalia akamuona nyoka
anaondoka akajua ameuumwa, haraka akarudi nyumbani akatoa taarifa.
Bi. Amina amesema akakimbizwa kwa
Mzee Shaban Makonga alipofika akatoa maelezo akachanjwa na kutolewa meno,
akapewa dawa ya kunjwa akatapika na kuharisha siku mbili tu mguu ulionza
kuvimba ukapona kabisa.
Mwisho.
0 Comments