Jumla ya Wanafunzi 15 kati ya wanafunzi 69 wa Shule
ya Sekondari Sepuka Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wamefaulu mitihani yao ya kidato cha nne mwaka 2023.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na makamu wa Mkuu wa Shule hiyo Abubakari
Amasi zinasema mwaka 2023 wanafunzi 69 walifanya mitihani ya kidato cha nne
waliofaulu vizuri ni wanafunzi 15 katika viwango vya division ya kwanza hadi ya
tatu.
Mwalimu Amasi anasema katika taarifa yake kuwa
kiwango cha division ya nne wanafunzi 47 walichaguliwa na wanafunzi 7 wapeta
division 0.
Katika taarifa yake mwalimu Amasi alibainisha kuwa
katika division ya kwanza wanafunzi 2 wamefaulu, katika division ya pili
waliopita ni mmoja na katika division ya 3 wanafunzi waliofaulu ni 12 hivyo
division ya 4 ni 47 na mwisho division ya 0 ni 7.
Shule ya sekondari ya Sepuka ilipata namba ya
usajili 797 mwaka 1998 ina walimu 16 kwa miaka miwili mfululizo 2020-2021 ufaulu
ulikua mdogo na shule kuapata alama ya kiwango hali hiyo iliwafanya wazazi na
wadau waanze kulalamika ufaulu ulikuwaje na kitu gani kilisababisha.
Wazazi na wadau wa elimu wamesema viwango katika
shule hiyo vilichukua miaka miwili lakini sasa shule iliweka mikakati
kuanzisha kambi mapema kuanzia mwezi Juni hadi Sept 2023 kwa maelezo ya uongozi
wa shule ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi watakaofanya mitihani walimu na
wanafunzi wakajibidisha katika masomo yao yote na matokeo yakawa mazuri.
‘‘Mwaka 2023 na mwaka huu walimu na
wanafunzi watafanya bidi kuongeza ufaulu na shule inategemea kuweka kambi
mapema ili wanafunzi wafaulu vizuri masomo yao.” Alisema mwalimu Amasi
Wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo wamefurahi mno
kuona Watoto wao wamefaulu kuendelea na masomo shule za juu hivyo wamewataka
walimu kuongeza bidi katika ufundishaji.
Walimu wa shule hiyo wamewataka wanafunzi waongeze
bidi kusoma masomo yao ili matokeo yam waka huu 2024 yawe mazuri Zaidi kuliko
mwaka uliopita wamewataka wapambane masomo yao kufaulu hawataki kuona shule yao
inapata alama ya ziro kwa wanafunzi.
Shule ya Sekondari Sepuka yenye walimu 16
ikishirikiana na wazazi na wanafunzi wa shule hiyo jitihada zao zimeongezeka
ufaulu kuliko mwaka uliopita hasa baada ya kuweka kambi miezi4.
Mwaka huu 2024 shule hiyo imepanga kuhakikisha
ufaulu unaongezeka kwa wanafunzi wengi kwa sababu walimu wamepanga kuweka kambi
mapema ili wanafunzi wapate muda wa kutosha na kuelewa masomo ili waje kufanya
mitihani yao.
Wazazi wametoa raia kwa serikali kwamba uanzishwaji
wa kambi kwa madarasa yenye mitihani ya kitaifa ni moja ya nja kuu ya kuongeza
ufaulu kwa wanafunzi wa madarasa hayo basi serikali iridhie na iweke wazi
ifahamike na itumike na wao hawana kipingamizi.
Nao wadau wa elimu wamesema shule ni viwanda
vinavyozalisha bidha bora, walmu ni mashine na wanafunzi ni malighafim za
viwanda na ili zizalishane bidhaa bora ni lazima serikali isimamie vizuri
mazingira yake.
0 Comments