Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Mhe Elia Digha akifunga kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliyopo katika mjimdogo wa Ilongero.
Baada ya jumuiya ndogo ndogo kushindwa
kujiendesha katika mradi wa maji vijijni ikiwamo kulipa mishahara,umeme na Wizara
ya maji nchini imetoa muongozo kwa mameneja wa ruwasa kuhakikisha wanaunganisha jumuiya zote kwa
lengo la kuleta tija na kupunguza usumbufu kwa watumiaji wa maji hasa vijijini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Ruwasa Halmashauri
ya Wilaya ya Singida Eng Athumani Mkalimoto
wakati akitoa taarifa ya Wakala wa Maji
na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA katika kikao cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mkalimoto amesema kuwa kwa Wilaya ya
Singida mpaka sasa kuna zaidi ya jumuiya 23 hivyo basi jumuiya hizo
zitaunganishwa kutoka 23 na kubaki na jumuiya 8 tu, ambapo amewata madiwadi
kuunga mkono hatua hiyo kwani inalengo la kuboresha huduma ya maji.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na
madiwani hao wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya mfumo huo mpya uliotolewa na
Wizara ya maji nchini Eng Mkalimoto amesema tatizo kubwa lililo jitokeza ni baada
ya ubadhirifu wa fedha uliotokana na wafanyakazi wa jumuiya hizo kushindwa
kusimamia miradi hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Singida Mhe Elia Digha akifunga mkutano huo
amewataka watendaji na watumishi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia mapato
ili kufikia malengo ya mapato waliyojiwekea.
0 Comments