Edwin Christopher Mwenyekiti wa Singida Veteran na Mratibu wa Bonanza la Pasaka.
Eva Pascal Mwenyekiti wa Singida Veteran Netball akiongea juu ya maandalizi ya Bonanza la Pasaka kwa upande wa Mpira wa Pete Netball.
Said Mustafa katibu wa Singida Veteran (SIVET) lengo la bonanza hili la Siku kuu ya Pasaka ni kujenga umoja wa timu za Veteran Mkoani Singida
Mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Gondwe anatarajiwa kuwa mgeni
rasimi katika bonanza la kusherehekea sikukuu ya pasaka,bonanza hilo
linaloratibiwa na timu ya Veteran Singida litakutanisha timumbalimbali
kutoka Mkoani Singida na viunga vyake.
Akiongea na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya bonanza hilo Edwin Christopher amesema kuwa kwa mawaka huu
hawata safari nje ya Mkoa kama ilivyozoeleka na wameamua kufanya
bonanza maalum la Pasaka na pia wamemuomba mkuu wa wilaya Godwin gondwe kuwa
mgeni rasimi katika bonanza hilo.
Christopher amesema kuwa bonanza hilo litakuwa na michezo ya
mpira wa miguu na mpira wa pete yani Netball likichagizwa na burudani
mbalimbali na nyama choma vyakura mbalimbali na kwa wale waliofunga mwezi
mtukufu watakuwa na chakura maarum baada ya mfugo kuanzia saa 1:00 jioni.
Naye katibu wa Veteran Singida (SIVET) Saidi Mustafa amesema
kuwa Lengo la bonanza hilo ni kutengeneza ushirikiano baina ya timu mbalimbali
za Veteran ambazo zinapatikana katika Mkoa huu wa Singida.
0 Comments