Mjumbe wa baraza Wazazi Taifa Varelian Kimambo akiongea na wananchi wa kijiji cha Mjura Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa Singida akiongea na Viongozi wa chama Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Singida Vijijini Alekzanda Mbongho akiongea kabla ya Mgeni Rasimi.
Wananchi wa Kijiji cha Mjura wakifuatiia mkutano.
Wanawake wameshauriwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za serikali za mitaa ili kuisaidia jamii kuzisemea changamoto zao nakuleta usawa wa kijinsia katika uongozi..
Ameyasema hayo mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya UGHANDI Wilaya ya Singida Vijijini wakati wa kuadhimisha Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
Nakomolwa amesema ili changamoto za jamii ziweze kutafutiwa ufumbuzi kwa wanawake wanatakiwa kuwa katika nafasi hizo ambazo wanaume wanazishika na kuchelewa kuzisemea baadhi ya changamoto.
Katika hatua nyingine amewataka Madiwani na Watendaji wa Kata kuwasomea Taarifa za Mapato na Matumzi Wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwani Serikali inatekeleza Miradi mbalimbali kwa kutumia Fedha nyingi hivyo ni muhimu Taarifa za Mapato na Matumzi ziwe wazi.
Aidha amewataka Wazazi kuhakikisha wanapinga Ndoa za utotoni kwani kumuozesha mtoto ni kufanya kitendo cha Ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ambao wanatakiwa kusoma na sio kuwa Mama wa familia.
0 Comments