Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema swala la watoto kwenda shule ni sheria ya nchi hivyo ni lazima viongozi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wote wanaopaswa kuanza shule ya awali, msingi na sekondari wanaenda shule.
Serukamba ameyasema hayo alipotembelea Wilaya ya Manyoni kata ya Kitaraka kuangalia zoezi la uandikishaji shuleni ili kuhakikisha kila mtoto anapata shaki ya msingi ya kupata elimu.
Amewaagiza viongozi kwenda kuwasaka watoto wote ambao hawajaandikishwa shule na kuanza taratibu za kuwachukulia hatua wazazi ambao wamewaficha watoto wao.
Aidha mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemilembe Lwota amesema ni jambo la fedheha kwa Wilaya hiyo kuwa wa mwisho katika zoezi la uandikishaji watoto shule na kuagiza viongozi wanaohusika na swala hilo kuandika barua na kueleza sababu za wao kutofuata maelekezo.
Hata hivyo mratibu elimu wa kata hiyo Cosmas Malamsha, afisa elimu Wilbert Chitanda na Mwenyekiti wa kijiji cha Dorotho wamesema changamoto kubwa ni baadhi ya vitongoji kuwa ndani ya mbuga ya Tanganyika Pakers ambapo miundombinu ya barabara sio rafiki hasa kwa kipindi hiki cha mvua na umbali mrefu wa shule ilipo.
0 Comments