WAKAZI WA KINDAI SINGIDA WAIDAI SERIKALI KWA ZAIDI YA MIAKA 39.

 


Maelezo ya picha.Naibu waziri wa ardhi.Geofrey Mizengo Pinda wa pili kulia (kutoka kushoto,akionyesha ramani ya viwanja eneo la Kindani manispaa ya Singida.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,Paskaz  Muragili na wa tatu kushoto ni Sumbu Alli Itambu. 

JUMLA ya wakazi 43 wa kata ya Kindai manispaa ya Singida mkoani hapa,wanaidai serikali mamilioni ya fedha kutokana na kupisha ujenzi wa reli na nguzo za umeme kwenye maeneo yao kwa zaidi ya miaka 39 hadi sasa.

Kwa mujibu wa maelezo yao wakazi 25, wanalidai shirika la umeme Tanzania (TANESCO) ,huku wengine 18 wakilidai shirika la Reli.Watu hao wanaodai fidia (jumla ya fedha hazijatajwa),ni pamoja na Chief Mughenyi Senge  Mughenyi, maarufu kwa jina la Ndovu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Misuna na mzaliwa wa kata ya Kindai,Shaban Omari Lesso,amesema kwa kipindi hicho kirefu wamekuwa wakizungushwa na wakati mwingine wanaambiwa ardhi haiana fidia.

“Nitumie fursa hii kumshukru Rais wetu msikivu Dk,Samia Suluhu Hassan,kwa kumtuma waziri wa katiba na sheria balozi Dk.Pindi Hazara Chana (mb),kuja mkoani Singida kuzindua kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria.Kupitia kampeni hii,tulio wengi tumepata ufahamu mpana wa kudai haki zetu kwa ujasiri mkubwa”,amesema.

Shaban ambaye pia ni makamu mwenyekiti taasisi ya mwalimu Nyerere manispaa Singida mjini,ameongeza kwamba kampeni hiyo ya mama Dk.Samia,itapungua udhulumaji au itakomesha kabisa.

Katika hatua nyingine,alisema wameshangazwa kuambiwa eti ardhi haifidiwa wakati katiba ya Taifa ibara ya 24 kifungu kidogo cha kwanza,imeelekeza mtu anastahili kulipwa fidia ya mali yake.

“Kila mtu ana haki ya kumiliki mali na hifadhi kwa mali zake aliyonayo,kwa mujibu wa sheria.Pia ibara hiyo hiyo kifungu cha pili,katiba inaagiza ‘Bila kuathiri mashariti ya kwanza,ni marufuku mtu kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kutaifishwa au madhumuni mengineyo, bila idhini ya sheria ambayo inayoweka mashariti.’

Aidha Shaban,amesema endapo fidia ya ardhi itashindikana kulipwa,basi serikali iwalipe  wananchi hao fidia za mali za kudumu zilizoathirika kwa zoezi hilo.

Ametaja baadhi ya mali hizo,kuwa ni pamoja miti aina ya miembe,mbao,mikalatuzi,mipera.Mali zingine ni mashamba ya kudumu na makazi yao.

Katibu kata Kindai Ibrahimu Mughuira Muro,amesema wananchi wengi kwenye kata yake,wameonewa na kunyang’anywa ardhi zao,kwa kutokujua sheria.

Bila kufafanua,amesema sheria ya nchi hii,zinatambua ardhi ni mali ya wananchi.Na msingi wo wote wa utawala,lazima upate ridhaa kutoka wa wananchi na si vinginevyo.

Desemba 12 mwaka 2023, naibu waziri wa ardhi Geofry Mizego Pinda, kwenye eneo hilo hilo la Kindai,alifanikiwa kuupatia ufumbuzi wa kudumu mgogoro wa ardhi.

Mgogoro huo ulimhusiha Sumbu Alli Itambu ambaye alikuwa anadai eneo lake limepitiwa na reli.Baada ya kufafanuliwa na afisa ardhi  manispaa ya Singida,Christian Kasambale.Pia alionyeshwa  ramani ya viwanja katika eneo hilo la Kindai.Mlalamikaji aliliridhia kuachana na mgogoro. 

Naibu waziri wa ardhi Pinda aliyepewa jukumu la kutatua malalamiko hayo na bosi wake,aliagiza Sumbu ambaye kwa miaka kadhaa amekuwa akilalamika kiwanja ni chake, sasa apewe kipau mbele kupata kiwanja kipya,na  ambacho atakipenda. 

Kuhusu watu wengine waliokuwa wakidai ardhi,aliagiza,“Hawa wananchi 47,kesho (jana 12/12/2023) hakikisheni mna waandikia barua za kuwatambua na na na kala, itufikie ofisini".aliagiza na kuongeza;

"Waahidini  wanaenda kupata viwanja vipya.Lakini watambue kwamba viwanja watakaopewa wasije wakasema vipo nje ya mji.Po pote pale kwenye eneo la manispaa,ni mji”,Amesisitiza.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments