MASHTAKA 601 YASAJILIWA MKOANI SINGIDA.


 Mkuu wa Mkoa Singida akiongea katika kilele cha wiki ya Sheria katika viwanja vya Mahakam ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida.


                                                      Mkuu wa mkoa wakati akiongea.


Mkuu wa Mkoa akiwasili na kupokelewa na Hakimu Mkazi Lau Nzowa na katibu tawala Dkt Fatma Mganga.



                            Mkuu wa Mkoa akiweka saini katika daftari la wageni ofisi ya hakimu mkazi


Mkuu wa Mkoa akipata  taarifa fupi kutoka kwa hakimu Mkazi Lau Nzowa baada ya kusaini kitabu cha wageni.



Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragiri akitoa neno katika kilele hicho cha siku ya Sheria.



Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Singida Mercy Ngowi akisoma  taarifa mbalimabli za ofisi hiyo katika kilele cha siku ya Sheria.



Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa katikati wakifuatilia matukio mbalimbali ikiwemo burudani ya muziki.

                                        

                                              Watumishi wa Mahakama wakiwa katika viwanja hivyo.

  

Viongozi wa dini mbalimali nao walikuwepo pia  na kutoa ushauri na maoni yao juu ya utendaji kazi wa vyombo vya Sheria nchini.

                                                
Picha ya kumbukumbu ya  meza kuu na viongozi wa dini.


                                         Burudani ya  Muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Kilima Band

Imeelezwa  kuwa Kwa kipindi cha Januari –Disemba mwaka 2023 Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka Mkoa wa Singida imeweza kupokea majalada 730 kutoka taasisi mbalimabali za kiupelelezi na kiuchnguzi na  baada ya kuyapitia na kuyafanyia uchunguzi wa kisheria wamefanikiwa kusajili mahakamani  jumla ya mashtaka 601.

Hayo yamejiri wakati wa kilele cha  Maadhimisho ya Siku na wiki ya Sheria Mkoani Singida yaliyofanyika katika viwanja vya  Mahakama ya Hakimmu Mkazi Mkoani hapo.

Akisoma taarifa ya utendaji kazi Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Singida Mercy Ngowi  amesema kuwa wamefanya vikao 13 vya Mahakama kuu ambapo walisikiliza kesi 175 zenye makosa ya mauwaji ,mauaji ya bila kukusudia,kujaribu kuua,kupatikana na madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa na Ugaidi.

Ngowi ameeleza kuwa  tume ya haki jinai inapendekeza baadhi ya maeneo kufanyiwa maboresho ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa mashahidi, kuondoa mamlaka ya ukamataji hovyo wananchi, kupitia upya makosa ya uhujumu uchumi na utaratibu wa kutoa dhamana na  kuweka ukomo wa upelelezi.

Aidha mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kilele cha maadhimisho hayo amewataka waendesha mashtaka kutoa haki kwa wakati na pia wanasheria kushauri namna ya kuwasaidia wananchi ili haki ipatikane kwa wakati.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments