KIMBUNGA na upepo
mkali ulioambatana na mvua kubwa umeng’oa mabati ya nyumba 9 na kuharibu nyumba
moja ya tembe Kitongoji cha Mayuyuda Kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi mkoani
Singida na kusababisha familia Zaidi ya 10 kukosa makazi japokuwa hakuna
aliyejeruhiwa lakini hasara kubwa imejitokeza uharibifu wa mali, mashamba na
nyumba zote zikiwa na thamani ya sh. 50 milioni.
Imeelezwa familia
za nyumba hizo hawana makazi wanaishi kwa ndugu zao baada ya nyumba 9 kati ya
10 kuharibiwa na kimbunga hicho kikali kilichofuatana na mvua tarehe 28/1/2024
saa 12:00 jioni na kuharibu chakula kilichokuwepo ndani ya nyumba.
Akitoa katika \kitongoji cha Mayuyuda Mwenyekiti wa Kitongoji
hicho Jumanne Ighembe amesema nyumba 9 paa zake zimeng’olewa na kimbunga hicho
siku hiyo jioni huku nyumba ya tembe imeharibiwa vibaya ba mvua na upepo wake.
Ighmbe amewataja
wanakijiji ambao nyumba zao zing’olewa bati ni pamoja na Shabani Kiseke nyumba
3, chakula gunia nne za mahindi na kuku 10 wamekufa.
Katika nyumba ya
Shabani Jafari bati zimeng’olewa, baiskeli na dram moja la lita 100 na wakati
huo huo nyumba ya Mzee Mussa Shabani imeng’olewa bati, baiskeli imeharibiwa na
migomba imevunjwa vunjwa yote.
Kwa mujibu wa
Ighembe nyumba Batuli Juma imeng’olewa na upepo magunia 2 ya mahindi
yameharibika, vyombo vya ndabni havipo, nguo hakuna na dramu
la plastiki la lita 100 limesombwa na maji.
Katika mkasa huo
nyumba mbili za bati za Mwanahamisi Masimba zimeezuliwa paa na upepo
mkali, nguo zimechukuliwa, mahindi gunia mbili na uwele, vyombo na
kitanda kimevunjika.
Katika taarifa
yake juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnang’ana Paskal Mdimi amesema
mashamba eka 25 za mazao mbalimbali yameharibiwa na upepo huo ulioambatana na
mvua kubwa.
Afisa Mtendaji wa
Kijiji hicho Skelita Kagaruki amesema gharama za nyumba zilizoharibiwa na
kimbunga iliyoambatana na mvua Kitongoji cha Mayuyuda ni sh. 35 milioni na
vyombo vilivyoharibiwa pamoja na kuku 10 ni sh. 5 milioni na mashamba ekari 25
zimeharibiwa vibaya hata hivyo tathimini yake haijajulikana.
Diwani wa Kata ya
Sepuka Halima Ng’imba ametoa pole wote waliopatwa na mkasa huo tareyhe
28/1/2024 nyumba zao kung’olewa na upepo huo uliosababisha uharibifu mkubwa wa
nyumba, chakula, vyombo na mashamba Zaidi y ash. 50 milioni
zinahitajika kuwasaidia waathirika katika kitongoji cha Mayuyuda
Kijiji cha Mnang’ana.
Mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha kila siku mkoani Singida mwaka huu 2024 zimeharibu
barabara zote za Moramu ndogo na kubwa vijijini, nyumba nyingi zimeharibika na
chakula yakiwemo mashamba ya mazao mchanganyiko ya chakula na biashara hata
hivyo maeneo mengine watafanikiwa kupata chakula cha kutosha lakini maeneo
baadhi yatakubwa na njaa kama hawatalima viazi na mihogo.
0 Comments