MWANAMKE mmoja mfanyabiashara ya samaki mkazi wa Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida Fatuma Juma (34) ameshambuliwa na kaporwa Mtoto wake wa mwaka mmoja na Salehe ambaye ni Mshikaji wake na Dereva wa pikipiki katika ugomvi wa kumgombania Mtoto na nyumba wanayoishi.
Wakizungumza wakazi wa kijiji hicho Fadhili Juma na Hamisi
Ramadhani walisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku Mabandani Kaugeri
kati ya Fatuma na Salehe wakimgombania mtoto na baadaye likajitokeza la
kugombania nyumba wakati Salehe alimkuta Fatuma ana nyumba hiyo.
Wakazi hao
walisema ugomvi wa watu hao wawili, Mama alikataa mtoto asichukuliwe kwanza
ananyonya na bado mdogo ana mwaka mmoja tu lakini Salehe anadai amchukue kwa
nguvu katika vuta nikuvute wakiwa mabandani Salehe akashirikiana na Hanje ambae
ni Shemeji yake wakaanza kumshambulia Fatuma.
Habari zinasema
watu hao wawili kwa pamoja wakaanza kumshambulia Fatuma kwa nguvu kwa kumpiga
kwa nia ya kutaka kumpora mtoto hadi Fatuma akazimia masaa 10 akazinduka kituo
cha afya Sepuka akipata matibabu.
Habari zaidi
zinasema watu walikusanyika kuamua ugomvi huo kati ya Fatuma na Salehe
wakawakamata Salehe na Hanje wakawapeleka ofisi ya kijiji kwa Mtendaji wa
kijiji kwa mahojiano, Maelezo mengine ya ufahamu na maamuzi lakini watu hao
waliachiliwa katika mazingira tata hivyo Salehe akapata nafasi ya kutosha
akaondoka na mtoto hajulikani alikokwenda hadi sasa na mtoto alikuwa anaumwa.
Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa kijiji hicho Robert Afungwe anasema mkazi wake Fatuma Juma
alipofika katika kijiji hicho miaka kadhaa ya nyuma alianzisha biashara ya
kuuza samaki akapata eneo la kiwanja akajenga nyumba baadae akanzisha mahusiano
na Salehe wakazaa mtoto mmoja ambaye sasa wanamgombania na imeelezwa Salehe
tangu afike 2019 anakaa na Fatuma akiwa boda boda.
Polisi wa kituo
cha Sepuka walimpokea Fatuma akiwa hoi amezimia kwa kushambuliwa na watu Wawili
mtu na Shemeji yake wakampa hati ya matibabu kuenda kituo cha afya Sepuka na
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho. Dkt Kessiah Mhina amethibitisha
kumpokea Fatuma Juma akiwa hana fahamu amezimia na baada ya jitihada za waganga
sasa anaendelea vizuri.
0 Comments