KUTOKANA na mvua kubwa zinaoendela kunyesha mkoani
Singida mwaka huu zimesababisha baadhi ya maeneo kuwa visiwa vya nchi kavu
kutokana na kuzingirwa na maji nyumba nyingi kuharibika na familia katika
nyumba hizo kupoteza maisha,mali na makazi.
Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Kipuma Kijiji cha
Masweya Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida. Tabu Lumanne Issaugo
(50) amekufa baada ya kuangukiwa na nyumba yake usiku wakati amelala baada ya
mwamba wa nyumba hiyo kuvunjika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Masweya David Hougoa
alisema kuwa Mwanamke huyo aliangukiwa na nyumba yake usiku baada ya mwamba wa
nyumba kuzidiwa uzito wa udongo wenye maji baada ya Mvua kubwa kunyesha.
Mwanamke huyo siku hiyo alikuwa pekee yake ndani ya nyumba hiyo ya iliyoezekwa kwa nyasi (Tembe) mwamba wa kati wa nyumba hiyo ulivunjika usiku wa manane ya saa 10:00 na majirani
waliposikia vishindo vya kuporomoka kwa nyumba hiyo walifika kutoa msaada kuta
zote zilibomoka hivyo udongo wa tembe, miti na majani yaliangukia ndani
alikolala Tbu. Alisema Hongoa.
Imeelezwa Tembe la nyumba hiyo lilikuwa na majani
mengi yameota juu yake udongo nao ulikuwa mwingi hivyo mwamba ulizidiwa nguvu
kutokana na uzito wa maji udongo na majani na miti nayo ilipinda hivyo tembe
lote lika mwaangukia. Tbu akapoteza maisha yake.
0 Comments