
Ndg
Rehema Sombi Afungua Tawi la wakereketwa kikundi cha Nguvu Kazi Bodaboda kata
ya Mwada wanufaika wa Pikipiki 5 kutoka kwenye Aslimia 4 za Halmashauri
zinazotokana na mapato ya ndani, amewaeleza Madhumuni ya Ziara kwamba ni
kuangalia Uhai wa Chama na Jumuiya zake, Kukagua Utekelezaji wa Ilani2020-2025
na Kuhamasisha Ushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa2024.
Na Kazi
yetu nyingine kama Umoja wa Vijana wa CCM ni kubaini Talanta za Vijana na
Kuwasaidia kufikia malengo kwa kuwatengenezea mazingira Rahisi ya Kuonyesha na
kunufaika na Taranta zao.
Nao
Bodaboda wa kata ya Mwada, Babati Vijijini Mkoani Manyara waomba Chama cha
Mapinduzi kiwape kipaumbele Vijana Katika kushiriki uchaguzi wa serikali ya
mitaa 2024. Hayo yamesemwa mbele ya Makamu m/kiti UVCCM Taifa Ndg. Rehema Sombi
alipofika kufungua Tawi la Wakereketwa kwa kikundi cha nguvu kazi.
Pia Amefikisha Salamu na Zawadi
ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh Dr. Samia Suluhu Hassan kwa Mamalishe wa Babati Vijijini kwa lengo la
Kuthamini mchango wao katika Kukuza na Kujenga Uchumi wa Taifa, na amenipa
zawadi hii ya vazi la mgahawani(Apron na kofia) niwaletee zenye ujumbe usemao(
Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu) .
Pia niwakumbushe kuchangamkia
Fursa ya Mikopo ya Halmashauri pindi itakapoanza kutolewa upya. Aidha
ametembelea Shule ya Sekondari Mbugwe na Kusomewa Utekelezaji wa Ilani ya CCM
2020/2025 kwa Kujengewa Madarasa, Madawati na Bwaro la Chakula pamoja na kutoa
Shukran za Dhati kwa Dr. Samia kwa Fedha za kukamilisha miradi hiyo. Hivyo Ndg.
Rehema Sombi amewasisitiza Wanafunzi wa Sekondari ya Mbugwe "Umuhimu wa
Kusoma kwa Bidii kuwaambia kwamba Dr. Samia Suluhu Hassan Ameendelea
kutengeneza Mazingira Rafiki ya kufundishia na Kujifunza.Kisha amefanya mkutano
wa hadhara kata ya Kisangaji.
0 Comments