Mwenyekiti wa Halmashari Mhe Elia Digha akifunga kikao cha Baraza la Madiwani la Halmshauri ya Wilaya ya Singida na kutoka na mkakati wa kukutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dotto Biteko.
Wajumbe wa kikao cha Baraza la Madiwani wakimsikiliza mkuu wa Wilaya.
Madiwani wakiwa katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mpya wa ofisi za Halmashauri Ilongero.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Singida limeadhimia kuonana na Waziri wa Nishati Mhe Dotto Biteko Ofisini kwake Jijini Dodoma kwa Lengo la kutaka kuomba kuongezewa idadi ya vitongoji vitakavyo patiwa umeme baada ya kupatiwa Vitongoji 15 tu kati ya Vitongoji 435 vilivyopo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Paskasi Muragili ameipongeza
Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa kuongeza bajeti ya Halmashauri kutoka 1.4b
mpaka 2.4b, amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa Mapato kwani Halmashauri inaweza kukusanya zaidi ya shilingi 3b na
kuvuka malengo mliyojiwekea.
Akiitaja mikakati hiyo Mhe. Muragili ameongelea Mradi wa Vikundi vya
Umwagiliaji ambapo tayari Maeneo Matano yanayofaa kwa shughuli hiyo yameainisha
na takribani visima 50 vitachimbwa ili kuwezesha utekelezaji wa mradi.
Muragili amewaomba Waheshimiwa Madiwani kuiongezea nguvu Idara ya Ardhi kwa
kutoa ajira za muda kwani nguvu kazi inahitajika katika Sekta ya Ardhi ili
kuwezesha sekata hiyo kuwa na mchango kwenye Mapato ya Halmashauri.
Akihitimisha hotuba yake Mhe Muragili amewataka Waheshimiwa Madiwani kupokea
Agizo la Mkuu wa Mkoa la kuwataka Wananchi wote wa Mkoa wa Singida kuwa na Choo
Bora ifikapo tarehe 30/04/2024.
0 Comments