Picha kutoka katika maktaba
MKAZI wa kijiji cha Nduluugu kata ya Ndulungu wilaya
ya iramba Mkoa wa Singida mmiliki wa mizinga ya nyuki 3,000 na bustani ya mboga
mboga na miti ya matunda eka 2 amekutwa amekufa kwenye kisima chake bustani
kwake akioga. Juma Athumani (48) huku mwili wake ukiwa hauna nguo, viatu, simu
nguo zake zikiwa juu ya tatu la kisima hicho.
Habari zinasema Juma Athumani (48) maarufu kwa jina la
“Mabuku”alikutwa amekufa saa 4;00 na mdogo wake Saidi Athumani na mwili wake
ukiwa unaelea juu ya maji ikidaiwa alifika hapo kwenye bustani yake kwenda
kuoga kwenye moja ya kisima chake akitokea mnadani Sepuka Jumanne iliopita.
Saidi Athumani amesema juzi kuwa alikwenda kwenye
bustani ya kaka yake kukagua kupata mboga na matunda saa 4:00 asubuhi kwanza
akaiona na nguo zikiwa juu ya tuta, viatu na simu janja akajua anaoga lakini
alipokaribia akauona mwili wa mtu ukiwa umeelea juu ya maji ya kisima hicho ni
wakaka yake hapo hapo akili ikahama mahali pake,mapigo yakazidi nguvu akaanguka
chini akapoteza fahamu akijua kaka yake amekufa saidi alichukua saa nzima
nchini alipopata fahamu kidogo akautazama tena akapiga yowe la nguvu watu
waliokuwa wakilima mbugani wapiti njia na wale wanaong’olea majani kwenye
majaruba ya mpunga walisikia yowe wakafika kujua kuna nini kimetokea kwenye bustani
ya mwenzao Juma Athumani walipofika na kumkuta Saidi analia mwili wa mtu ukiwa
juu ya maji ukiwa hauna nguo wakatazama pikipiki, nguo,viatu na simu wakapata
majibu ya maswali yao kwamba mwenye bustani hiyo na pikipiki hiyo amekufa na
wao wakasaidia kupiga mayowe na kutoa taarifa kwa viongozi wa kijij na kata.
Mwenyekiti wa kijiji anasema amesikitishwa sana na
kifo cha Juma Athumani “MABUKU” ambae ni mkazi wa kijiji chake mkulima na
mmliki wa mizinga ya nyuki 3,00 yenye nyuki amepoteza maisha akioga kwenye
kisima chake akitokea mnadani sepuka.
Viongozi wa kata walipofika na kushuhudia baada ya
kupata taarifa hizo walisilikitika sana wanasema marehemu alikuwa mfano mzuri
kwa wakazi wa kata hiyo alihamasisha ulimaji wa mboga mboga na utunzaji nyuki
ili kuondikana na umasikini kirahisi kwa kutumia fursa zilizopo kwenye makazi
ya watu.
Viongozi walitoa taarifa Polisi Ndangu na Kiomboi na
walipofika walifuatana na waganga walifanya uchunguzi wa mwili wa Juma wakapata
maelezo kutoka kwa saidi , viogozi wa kijiji ,wa kata wakaridhia kuwa Juma
amefariki kisimani akioga na Ndugu zake azikwe. Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida kamishina msaidizi wa plisi ACP Stella Mutabihirwa
hakupatikana kwa simu yake hata hivyo tukio kama hili ni la kawaida kutokea
katika jamii.
Katika tukio jingine mifugo 20 imekufa kwa kupigwa na
radi saa 11:00 jioni siku ya jumatano wiki iliyopita ikitoka machungani baada
ya mvua kubwa kuanza kunyesha kwenye kijiji cha Nsonga kata ya
Kaselya wilaya ya Iramba Afisa mtendaji wa kijiji Remji John amesema mifugo
hiyo mali ya Athumani Mpondo ilikutwa na mkasa huo wakati ikirudi
nyumbani jioni hata hivyo amesema radi mara nyingi hutokiea mara kwa mara
kwenye eneo hilo.
Mwenyekiti wa kijiji Mujango Mdudi amesema mbuzi
5,kondoo 14 na ng’ombe 1 wamekufa kutokana na radi hiyo hakuna mtu
aliyejeruhiwa hivyo familia yam zee Athumani Mpondo imepata hasara kubwa kwa
kukosa mifugo 20.
0 Comments