WANAFUNZI 421 WA SHULE YA MSINGI IKUNGI MAGHARIBI KUJIUNGA NA SEKONDARI 2024


Justice Kijazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ya Wilaya ya Ikungi akiwa Ofisini kwake wilayani Ikungi.

JUMLA ya wanafunzi 421 wa shule ya msingi Musimi, Msungua, Mnang’ana na Italala kata ya Sepuka wilayani Ikungi Mkoa wa Singida wameanza masomo shule za Sekondari Sepuka na Msungua kufuatia kufunguliwa kwa shule hizo mapema Januari mwaka huu 2024 baada ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya shule hizo 2024.

Katika taarifa yake wakati akiongea na mwandishi wetu, Afisa Elimu Kata ya Sepuka Idd Kisuda amesema mwaka huu 2024 wanafunzi 421 wamefaulu kuingia kuanza masomo ya shule za Sekondari Sepuka na Msungua kati ya wanafunzi 507 waliofanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi 2023 ni sawa na asilimia 84 ambapo wanafunzi 86 wamefeli mitihani hiyo.

Afisa Kisuda amesema shule za msingi Musimi, Msungua, Mnang’ana na Italala hawakuweka kambi kwa wanafunzi wa darasa la saba ili kuongeze ufaulu, kwa wanafunzi wa shule hizo lakini ufaulu wao umetokana na wazazi wao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shule ya msingi musimi mwalimu Mkuu wa shule hiyo Nemesiana Remmi amesema wanafunzi 106 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2023 na waliofaulu ni 96 hivyo wanafunzi 10 hawakuchaguliwa kuendele na masomo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi italala Jumanne Hanti katika taarifa yake amesema wanafunzi 63 walichaguliwa kuendelea na masomo shule ya msingi 2023 hivyo wanafunzi 25 hawakuchaguliwa kuendelea na masomo ya shule ya Sekondari 2024.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Msungua Julius Lema katika taarifa yake alisema mwaka 2023 wanafunzi 183 walifanya mitihani ya kumaliza darasa la saba na waliobahatika kuchaguliwa kuendelea na masomo shule ya Sekondari Msungua ni 145 hivyo wanafunzi 38 wamefeli kuendelea na masomo 2024.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mnang’ana Mahendeka amesema katika taarifa yake kuwa mwaka 2023 shule yake ilikuwa ina wanafunzi 130 waliomaliza darasa la saba wakafaulu 117 hivyo wanafunzi 13 hawakuchaguliwa kuendelea na masomo katika shule za sekonadari.

Afisa Mtendaji kata ya Sepuka Hussein Kelinga amewateka wazazi wa wanafunzi waliochaguliwa kuendelea na masomo yao shule za sekondari zilizopo Sepuka wahakikishe wanawapeleka Watoto wote kuanza masomo yao bila kukosa na wazingatie maelekezo yote ya wakuu wa shule hizo katika fomu walizopelekewa.

Wazazi wa wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi katika shule za msingi kata ya Sepuka, Musimi, Mnang’ana na Italala wanatoa shukrani sana kwa walimu wa shule hizo mwaka uliopita 2023 kwa kufundisha kwa bidi masomo yote bila kuweka kambi hadi kufaulu vizuri kwa asilimia 84 na hii ni pamoja na wanafunzi wenyewe kuwa wasikivu wanapokuwa madarasani.

“Sisi wazazi tunataka waendelee na nia hiyo hiyo ili wafikie malengo yao watimize ndoto zao nasi tuko tayari kuwapa walimu na  Watoto ushirikiano wakutosha ili baadae taifa lipate viongozi bora na wenye elimu” walisema wazazi.


 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments