ALIYESOTA GEREZANI ZAIDI YA MIAKA 50 NAKUTOKA ASIMULIA.

                                                             

                                                                            Glynn Simmons 


                Glynn Simmons akwa na mwanasheria wake na ndugu na jamaa baada ya kutoka Mahakamani.

 Glynn Simmons alitazama nje ya dirisha kwa muda mrefu, alipoketi kwenye upande wa abiria katika gari ambalo rafiki yake alikuwa akiliendesha, wawili hao wakiwa kwenye barabara kuu ya kuelekea mji wa Tulsa katika jimbo la Okahoma. Macho yake yalikuwa yanalenga anga iliyojaa mwanga wa nyota katika usiku huo.

Ilikuwa hali ambayo mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 70 alikuwa hajashuhudia kwa takriban nuzu ya karne, kwani alikuwa gerezani akihudumu kifungo cha Maisha kwa kosa la mauaji ambalo hakulitekeza.

‘'Ni vitu kama hivi…kutazama misimu ikibadilika, majani ikiwa ardhini, mambo ya kawaida ambayo singeweza kuyafanya nikiwa gerezani. Hungeweza kuifurahia, hungeweza kuitizama, Simmons aliliambia BBC. ‘ Ni jambo la kusisimua sana.’'

Bwana Simmons aliachiliwa huru kutoka gerezani mwezi Julai mwaka jana {2023}. Mwezi Desemba, alipatikana bila hatia na kutangazwa asiyekuwa na makosa kwenye kesi ya mauaji ya Carolyn Sue Rogers iliyofanyika 1974.

Hukumu yake ambayo ilikuwa ya makosa, ndio iliyochukuwa muda mrefu zaidi katika historia ya taifa la Marekani.

Hukumu dhidi yake ilifutiliwa mbali, baada ya mahakama ya wilaya {jimbo} kupata ushahidi kwamba waendesha mashtaka kwenye kesi hiyo hawakuwa wamewasilisha ushahidi wote kwa mawakili wa upande wa utetezi, ikiwemo taarifa muhimu kwamba mmoj awa mashahidi alikuwa amewatambua washukiwa wengine.

Simmons alikuwa na umri wa miaka 22, wakati yeye na mshtakiwa mwenza Don Roberts walishtakiwa na kupewa adhabu ya hukumu ya kifo mnamo 1975, adhabu ambayo baadaye ilibadilishwa na kuwa kifungo cha maisha gerezani.

Simmons, alizungumza , wiki hii kuhusu maisha mapya akiwa huru, changamoto ya kiafya anayokabiliana nayo ya saratani iliyo katika kiwango cha nne, na imani na matumaini ambayo ilikuwa kiungo muhimu maishani mwake katika miaka 48 aliyokuwa gerezani.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments