MBUNGE WA IRAMBA MAGHARIBI NA WAZIRII WA FEDHA DKT MWIGULU NCHEMBA ATOA MITUNGI 900 YA GESI.

 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akiogea na waandishi wa Habari juu ya faida na matumizi ya Gesi.


Mkurugenzi Mkuu wa Gesi ya Oryx Nchini Benoit Araman akiongea na wanachi wakati wa makabidhiano hayo mjini Iramba.

.

Askari kutoka Jeshi la Zimamoto FC Rahma  Abdarabi aitoa maekezo kwa watumiaji wa gesi hizo ili kujikinga na ajali ya moto.

Matumizi bora ya jiko la gesi

                                                                            Mitungi ya Gesi 

Mkurugenzi Mkuu wa Gesi ya Oryx Nchini Benoit Araman akikabidhi mtungi wa Gesi kwa mkazi wa Iramba.


Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba Ametoa mitungi 900 gesi ya Kupukia kwa Wakazi wa Wilaya ya Iramba ikiwa ni Mkakati wa Kuhimiza Matumizi ya Nishati Mbadala ili kukomesha Matumizi ya Kuni na Mkaa ambayo yanachangia uharibifu wa Mazingira.

Akikabidhi mitungi hiyo kwa niaba ya Mbunge huyo, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda Amesema Zoezi hilo ni Kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wanatunza Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Gesi ya Oryx Nchini Benoit Araman Amesema  Matumizi ya Gesi yatasaidia kwa Kiasi Kikubwa Kulinda Mazingira na  kulinda Afya za watumiaji hasa Wanawake kwenye Mapishi kwani itawaepusha kuvuta Moshi unaoweza kuathiri  Mapafu.

Naye Askari kutoka Jeshi la Zimamoto FC Rahma  Abdarabi Amewatahadharisha Wananchi Juu ya Vitu Vinavyoweza Kusababisha Athari za Kulipuka kwa Gesi Pamoja na Namna ya Kudhibiti Moto ili Kuepusha Madhara kwao na Mali Zao.

Baadhi ya Wakazi wa Wilaya ya Iramba Ambao Wamenufaika na Zoezi hilo Wamemshukuru Mbunge wao kwa Kuwasaidia Nishati hiyo huku Wakiiomba Serikali Kuweka Ruzuku Katika Gesi ili kuwasaidia Kupata Nishati hiyo kwa Urahisi pale inapoisha.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments