WAKALA WA MBEGU NCHINI ASA KUSAMBAZA MBEGU YA ALIZETI TANI 2000 NCHINI 2023/2024.

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde na viongzi mbalimbali wa mkoa wa Singida akiwemo Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamba wakikata Utepe kwenye gari lililobeba Mbegu ya Alizeti kutoka kwa wakala wa Mbegu nchini ASA.



Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde  Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba na wakala wa Mbegu nchini Dkt Sofia Kashenge wakitazama mifuko ya Mbegu aina  Recoda zilizoletwa na wakala huyo ikiwa ni katika uzinduzi wa usambazaji wa Mbegu ya Alizeti mkoani Singida.


        Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba kushoto mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe Musa Sima katikati na Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu wakipokea Mbegu ya Alizeti.

                                  

                                          Vingozi wakibadilishana mawazo kabla ya kukata utepe.


Katika msimu wa kilimo 2023/2024 Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na wakala wa mbegu ASA inatarajia kusambaza mbegu bora za alizeti zenye ruzuku kwa Wakulima zaidi ya tani 2,000 nchini zenye thamani ya sh.bilioni 8.58.

 

Naibu waziri wa kilimo David Silinde ametoa taarifa hiyo wakati akizindua zoezi la usambazaji wa mbegu bora za alizeti zenye ruzuku kwa Wakulima Mkoa wa Singida ambapo Mkoa kwa msimu huu utapokea mbegu hizo tani 600.

 

Naibu waziri huyo amesema tangu wiraza kuanza utaratibu wa kusambaza mbegu bora za alizeti Uzalishaji umeongezeka hivyo akaziagiza Halmashauri kutoa ushirikiano kwa Wizara na wakala wa mbegu ili zoezi la usambazaji wa mbegu bora za alizeti liweze kufanikiwa kwa kuwafikia Wakulima wote.

 

 

Awali kabla ya kumkaribisha naibu waziri kuzindua zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ametoa maelekezo kwa Wakulima kutumia mbolea sio tu kwenye mazao mengine hata kwenye zao la alizeti ili waongeze Uzalishaji.

 

Pamoja na kuwataka wakuu wa Wilaya kwenda kusimamia suala la usambazaji wa mbegu amewataka Viongozi kwenda kusimamia makubaliano ya Serikali ya Mkoa ya kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa bei halali.

 


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments