MBUNGE WA SINGIDA ATEMBELEA HOSPITAL YA RUFAA YA MANDEWA NA KUKABIDHI GARI.

                             

                         Mbunge wa Singida mjini Mhe Musa Sima akikata utepe wa gari jipya kwa niaba ya Serikali.





                                              Mhe Musa Sima akiwasha gari jipya baad ya kukata utepe.

                               

                              Mhe Musa Sima akiongea na watumishi wa hospitali ya rufaa ya Mandewa mjini Singida.




                               Dr Davidi Mwasota Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mandewa akitoa taarifa ya  hospitali.



          Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida Yasinta Alute akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasimi.

                      

                          Picha ya kumbukumbu ya na mgeni rasimi na uongozi wa hospitali ya rufaa Mandewa.


                                       

                                             Picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya rufaa ya Mandewa

Mbunge wa jimbo la Singida Mhe Musa Sima ametembelea Maabara ya Hospital ya rufaa ya Mandewa na kujionea huduma zinavyotolewa katika hospitali hiyo,Sambamba na kukabidhi gari moja(1) kwa niaba ya Serikal kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya hospitali hiyo.

Sima alisema kuwa kuna haja ya hospitali hiyo kupata Madaktai bingwa kwa ajili ya huduma za kibingwa za Pua na Koo,Pamoja na kuwa na Madaktari bingwa wa maeneo mengine.

hata hivyo alisema Singida itatambulika kwa huduma ya eneo hilo la Pua na Koo kikanda na kitaifa pia.

Aidha alitoa wito kwa watoa huduma katika hospitali hiyo kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi wanao kuja kupata huduma katika hospitali hapo.

Awali akimkaribisha mgeni rasimi Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe Musa Sima kaimu mganga mkuu Yasinta Alute alishukuru Serikali kwa kuwapa gari hilo kwani litasaidia kupunguza adha ya usafiri kwa watoa huduma hasa katika ngazi za chini.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments