Magari yalivyo kwama katika barabara kuu kuelekea kijiji cha Gendabi wilaya ya Hanag na kusababisha msafara wa viongozi wa taasisi ya dini ya kiislam ya Jasunta kushindwa kufika huko kutokana na mvua zinazoendelea kunesha sasa.
Wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza na kwenda kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika Mkoa wa Manyara Wilayani Hanang na kugharimu maisha ya watanzania na mali zao.
Wakiendelea kuunga mkono kauli ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwasaidia wenzetu walipoteza ndugu zao, mali pamoja na makazi Umoja wa Mawakala wa Mabasi ya abiria yanayofanya safari za Mikoani stendi kuu Misuna Singida mjini umetembelea umetembelea eneo hilo na kutoa msaada.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dini ya kiislam ya Jamaalut Answar Sunn Tanzania (JASUNTA) Yahaya Mohamd Ibrahimu yenye makazi yake mkoani Singida na waumini wa dini ya Kiislam kutoka Mkoa wa Singida pia wamefika kutoa misaada yao,Taassi hiyo Imetoa Mabelo 17 ya Nguo,Kilo 550 za Unga,Sabuni,Mafuta ya kupaka na Dawa za Meno. huku wakitoa wito kwa watu wengine kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja baada ya kupokea misaada hiyo amewashukuru wadau hao na kueleza kuwa Kazi ya maandalizi ya Ujenzi wa nyumba za makazi inakwenda kuanza Mara moja kwani eneo lipo tayari na vifaa vipo.
0 Comments